Mchezo kati
ya Mtibwa Sugar na Simba Juzi ulioipa ushindi Simba Sc katika Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Mtibwa Sugar 1-0 Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro umemsababishia majeraha kijana mmoja mjini Babati.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Manyara akizungumzia tukio hilo ameeleza kuwa limetokea tarehe
9.4.2018 saa tatu usiku ambapo Mtuhumiwa huyo aliefahamika kwa jina la Stefano Festo
[35] mkazi wa Hangoni C alimjeruhi mhudumu wa Bar ya Toroka Uje mtaa wa
Osterbay Daniel Elia baada ya kuzuka mabishano
ya ushabiki wa mpira mechi kati ya
Mtibwa Suga na Simba Sc .
Kijana huyo
ambaye ni shabiki wa Simba alikuwa akishangilia ushindi walioupata jambo ambalo
lilimkera Daniel anaeaminika kuwa ni
shabiki wa Yanga na kuamua kumponda kwenye paji la uso na mtwangio wa Kinu na
kumsabishia Maumivu makali.
Kamanda
Senga amesema mtuhumiwa bado anashikiliwa katika kituo cha polisi mjini Babati
kwa hatua nyingine za kisheria.
Daniel
aliejeruhiwa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya
mji wa Babati Mrara.
Ushindi huo wa juzi unaifanya Simba SC ifikishe pointi 52 katika mechi ya 22 ikiendeleza kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21, wakati Mtibwa Sugar inabaki katika nafasi ya sita na pointi zake 30 za mechi 22 pia.
Ushindi huo wa juzi unaifanya Simba SC ifikishe pointi 52 katika mechi ya 22 ikiendeleza kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21, wakati Mtibwa Sugar inabaki katika nafasi ya sita na pointi zake 30 za mechi 22 pia.
Bao hilo
lilifungwa na mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi dakika ya 23 kwa shuti
akiwa ndani ya boksi baada ya pasi ya kichwa ya Nahodha John Raphael Bocco
aliyeunganisha krosi ya winga Shiza Ramadhani Kichuya.
Post a Comment
karibu kwa maoni