Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, imesema inakusudia kumpeleka msanii Nandy
polisi juu ya video yake ya utupu iliyovuja.“Tulitunga sheria toka mwaka 2010 lakini tulikosa kanuni, na sasa hivi tumeshaweka, na zimeshaanza kufanya kazi, jana tumempeleka mahakamani msaniii Diamond kwa video alizorusha, na pia Nandy itabidi apelekwe polisi kuhojiwa”, amesema Waziri Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe ameendelea kwa kuwataka vijana kutotumia mitandao ya kijamii vibaya kwani mitandao sio kokoro ya kupeleka uchafu wowote, kwa kuwa nchi ina maadili na utamaduni wake na inapaswa kuulinda.
Post a Comment
karibu kwa maoni