Rais
John Magufuli amekumbushia jinsi ambavyo msimamo na uimara wa rais
mstaafu, Jakaya Kikwete ulivyomuwezesha kuingia Ikulu mwaka 2015.
Akizungumza
jana Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya ufunguzi wa taasisi ya
Jakaya Kikwete, Rais Magufuli alisema kuwa hataacha kumshukuru kila
wakati wanapokutana bila kujali.
“Kwako
Kikwete napenda kukuahidi kuwa nitaendelea kukushukuru kila
tutakapokutana, ukichukia, ukifurahi mimi nitakushukuru kwa sababu wewe
ndiye uliyesimama imara mpaka leo hii mimi ni Rais,” alisema rais
Magufuli.
Aidha,
alitambua mchango wa Kikwete katika kuleta maendeleo ikiwa ni pamoja na
ubora wa miundombinu uliofanyika wakati wa akiwa rais.
Alisema rais huyo mstaafu katika awamu yake alifanya mengi ikiwa ni pamoja na kujenga shule za kata, barabara na hospitali.
Alipongeza pia uanzishwaji wa taasisi ya Jakaya Kikwete ambayo imejikita katika masuala ya afya, vijana na utawala bora.
Rais Magufuli aliahidi kuwa serikali yake itaiunga mkono taasisi hiyo kwani ina tija katika sekta zote inazohusika nazo.
Akizungumzia
taasisi yake, Kikwete alisema kuwa pamoja na mambo mengine, imelenga
kuwasaidia vijana kuwapa mafunzo ili wawe na elimu, wazalendo na wenye
maadili mema wakitumia akili na nguvu zao kujiletea maendeleo.
Post a Comment
karibu kwa maoni