Wanafunzi wawili wakazi wa Olkeryan jijini Arusha
wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo lililokuwa likitumika
kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mchepuko inayotoka Ngaramtoni
kuelekea Moshono.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo jana
Jumatano Aprili 11, 2018 aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Hadija Hans
aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Olkeryan na
Christina Kivuyo mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Mt Meru.
Mkumbo alisema Hadija alikuwa akipita karibu na shimo hilo
hilo Jumanne saa 11;30 jioni na kutumbukia na kwamba Kivuyo
alipokwenda kwa nia ya kumsaidia naye alitumbukia katika shimo hilo na
wote kufariki dunia.
Amesema baada ya tukio hilo wafanyakazi wanaojenga barabara
hiyo kwa kushirikiana na wananchi na polisi walienda eneo la tukio na
kukuta miili ya wanafunzi hao, ambayo waliipeleka Hospitali ya Mt Meru.
Post a Comment
karibu kwa maoni