Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa
kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, zijulikanazo kwa jina la The
African Prestigious Awards zinazotarajia kufanyika nchini Ghana.
Taarifa
hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk.
Harrison Mwakyembe wakati akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini
Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana
katika tuzo hizo ambapo ameweka wazi kwamba Tanzania imepata heshima
kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika.
Amesema
kuwa Utendaji uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo
vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious
Awards.
“Tanzania
imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara
la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika,
napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King
Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika" Dkt.Mwakyembe.
Ameongeza
"Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na
Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja
na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora
Afrika".
Monalisa
anatarajia kuondoka nchini mapema wiki hii kwenda nchini Ghana kwa
ajili ya Tuzo hizo ambapo amewaahidi watanzania kuwa lazima atarudi na
tuzo kwani anawawakilisha wasanii wenzake hao wawili pamoja na mpiga
picha huyo aliyetajwa na pia aliishukuru serikali kwa kumpatia tiketi
kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni