0
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wameshindwa kuhudhuria harusi ya mwanamuziki wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba anayefunga  ndoa na mchumba wake, Amina Rikesh kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Hayo yameleezwa na mtoto wa Rais Kikwete na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa mjini Dodoma anapohudhuria vikao vya Bunge.

Ridhiwan amesema kuwa, walipewa mwaliko wa kuhudhuria harusi ya mwanamuziki Ali kiba, lakini Rais mstaafu Kikwete kwa sasa anahudhuria shughuli nyingine Marekani, naye Ridhiwani anahudhuria vikao na shughuli mbalimbali bungeni mjini Dodoma hivyo hawataweza kuhudhuria harusi ya mwanamuziki huyo Kenya.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top