Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Martin Busungu amesema
gharama za ujenzi wa ukuta wa mgodi wa Tanzanite, ni Sh5 bilioni.
Jenerali
Busungu amesema ukuta huo wenye kilometa 24.4 utazunguka eneo lote la
mgodi wa Tanzanite na tathmini ya awali, ilionyesha kwa kilometa 21
zingetumika Sh 4 bilioni.
Akizungumza leo Aprili 6 katika uzinduzi wa ukuta huo, Busungu amesema vikosi 20 vya JKT vimejenga ukuta huo.
“Tumetekeleza
kwa uadilifu na uamnifu ujenzi huu. Tunatoa shukran za dhati kwa
taasisi za uhandisi Tanzania kwa ushirikiano wao,” amesema
Amesema Jeshi la JKT lipo tayari kutekeleza maaagizo yoyote yakatayotolewa kwa mustakabali wa Taifa.
“Hata
hivyo kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwamo ugumu wa ujenzi hasa
katika miamba, uwepo njia za nyingi za maji ambazo hata hivyo wahandisi
wa Pangani River walisaidia,” amesema
Leo
Rais John Magufuli anazindua ukuta huo. Viongozi mbalimbali, wakuu wa
mikoa, wa wilaya na mawaziri wamehudhuria hafla hiyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni