0

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Tabora imemkata na kumfikisha Mahakamani askari mgambo kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Tabora, Mogasa Mogasa amesema mtuhumiwa Pascal Edward Gapi amekamatwa Aprili 17, 2018 na kufikishwa Mahakamani baada ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja kutoka kwa msamalia mwema akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Aidha, Mogasa amesema kuwa mtuhumiwa huyo kwa kushirikina na mwenzake ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Nyasa Siri John Mboya walitenda kosa hilo Julai 10, 2014 ili waweze kuwapatia dhamana na kuwafutia kesi watuhumiwa watatu wa kesi ya jinai namba 140/2014 iliyofunguliwa Mahakamani hapo.
Hata hivyo Mogasa amesema kuwa baaada ya kukamatwa kwa Pascal Edward mtuhumiwa wa pili ambae ni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Nyasa amekimbia hivyo Takukuru mkoani humo inaendelea kumsaka ili aweze kuunganishwa na mwenzake katika shitaka hilo .
Wakati huo huo  bwana Mogasa amesema Takukuru mkoani humo  imempandisha pia kizimbani Afisa mtendaji wa kijiji cha ukondamoyo bwana Ramadhani Saidi Mbeleke  kwa  tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi laki tano na tisini elfu .

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top