0
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia mbele ya mashabiki 5,000 katika dimba la Stadio OlimpicoLiverpool imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tokea 2007 kwa jumla ya magoli 7-6 licha ya kupoteza mbele ya Roma kwa magoli 4-2.
Safari ya Liverpool ilianzia Ujerumani Agosti 15 ilipocheza na Hoffenheim na May 26 itachuana na Real Madrid mjini Kiev.
Licha ya kupoteza katika mchezo huo, ilikua shangwe kwa mashabiki wa Liverpool 5,000 waliosafiri kuhakikisha timu yao inapata nguvu ya ziada kutoka kwao kwenye dimba la Stadio Olimpico.
Klopp alikumbatia kila mchezaji wakati timu yake ikipiga picha ya pamoja baada ya mchezo.
Mashabiki wa Liverpool waliendelea kushangilia kwa nguvu hata baada ya mchezo kwisha huku wakisalia kwenye jukwaa lao.
Wakiwa na faida ya magoli 5-2 katika mzunguko wa kwanza nyumbani Anfield, Liverpool ilianza kujipatia goli lake kupitia Sadio Mane baada ya pasi safi ya Roberto Firmino.
Magoli mengine yalifungwa na Georginio Wijnaldum, James Milner, Edin Dzeko, na Radja Nainggolan akipachika mawili.
Livepool itachuana na Real Madrid katika fainali ya May 26 mjini Kiev, Ukraine.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top