Mfanyabiashara mmoja mjini Mbulu, Abie Tara amejitolea
kuwasaidia vijana kuepika matumizi ya pombe kwa kuanzisha ligi ya mpira wa
miguu.
Wakizungumzia michuno hiyo wakazi na viongozi wa timu
wameelezea ligi hiyo ambapo leo Sanu Baray ilimenyana na Bargish katika hatua
ya nusu fainali.
Mchezo wa leo ulikuwa wa kusisimua timu zote
zikionyeshana ubabe dakika 90 za mchezo.
Ilimlazimu mwamuzi kuongeza dakika 30 lakini bado hali
ilikuwa tete hivyo kuwapeleka katika matuta.
Sanu baray [Chama cha wana] ilipata penati 1 kati ya tano ilizopata huku
Bargish akipenya katika hatua ya Nusu fainali kwa kupata penati 5.
Kocha wa Bargish Emmanuel
Bayo alisema licha ya wapinzani wao
kutamba kwa mipira mingi ya kichwa lakini Ubingwa unakwenda kwao.
Sasa Bargish alieingia leo katika hatua ya Fainali
anakutana na madereva Boda boda kutoka kijiwe cha Manji.
Mmoja kati ya mashabiki wa Sanu Baray Mama Ante ametupa
lawama zake kwa waamuzi wa mchezo huo akieleza kuwa wamebebwa baada ya
wapinzani kuwafanyia madhambi eneo la penati na mwamuzi wa kati kupotezea
adhabu hiyo ambayo ilikuwa ni penati.
Post a Comment
karibu kwa maoni