
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Jacqueline Ngonyani ‘Msongozi’ ametoa chozi
bungeni akiitaka Serikali kuwalipa mawakala wa pembejeo na kuacha
kutumia kivuli cha uhakiki wa madeni hayo kutoyalipa.
Akichangia
bajeti ya kilimo, leo Mei 15, 2018 bungeni, Msongozi amesema madai hayo
yamedumu kwa zaidi ya miaka minne huku baadhi wakifariki kabla
hawajalipwa.
“Nashangaa
sana mawakala wa pembejeo wanadai miaka minne, walihudumia wakulima
wetu na walikwenda kukopa fedha katika taasisi, ambazo sasa zinawadai,”
amesema Msongozi.
Huku
akishangiliwa na wabunge, Msongozi amesema, “Serikali imekuwa
inajificha katika kichaka cha uhakiki, kwa nini hawawalipi? Serikali
imekwenda kujificha katika uhakiki, ni uhakiki wa aina gani? Kuna watu
wanakufa bila kupewa fedha zao.”
Msongozi
akizungumza kwa sauti yenye kuashiria kulia huku mkono wake akiupeleka
kufuta uso wake, amesema, “katika nchi hii watu wanatafuta haki zao,
kama wameiba kwa nini wasipelekwe mahakamani, kwa nini hawapewi fedha
zao, uhakiki gani, mbona watumishi siku mbili walihakikiwa? Kwa nini
huku katika mawakala hawalipwi fedha zao.”
Amesema
kuna kijana alitaka kujinyonga kwa kudaiwa na taasisi jambo ambalo
amesema Serikali ichukue hatua ya kulipa madai kwani wako mawakala saba
wamepoteza maisha.”
Msongozi
amekuwa mbunge wa tatu kutoka CCM kutokuunga mkono bajeti hiyo
akitanguliwa na Richard Ndassa (Sumve) na Mashimba Ndaki (Maswa
Magharibi).
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.