
Serikali ya Uganda imeagiza kuanzia sasa vitabu vitakatifu vya Biblia na Quran vinavyoingizwa nchini humo vilipiwe kodi.
Viongozi
wa Kidini kutoka madhehebu hayo mawili makubwa nchini humo wamepokea
uamuzi huo kwa tahadhari kubwa na mshangao huku wakisisitiza kwamba,
vitabu hivyo vya kidini havipaswi kutozwa kodi kwani vinatumika kujenga
na kuimarisha imani za kiroho za wananchi wa Uganda.
Katibu
Mkuu wa Baraza Kuu la Waislaam Nchini Uganda, Ramadhan Mugalu,
ameikosoa serikali kwa kusema kuwa, hatua hiyo imevuka mipaka, na kuhoji
inawezaje kutoza kodi neno la Mungu?
Kwa
upande wake Kamishna wa Makanisa nchini humo, Mchungaji Joram Kahenano,
amesema Kanisa lake litalazimika kuongeza bei ya Biblia moja kutoka
shilingi za Uganda elfu tatu hadi elfu 18 ili kufidia gharama za kodi.
Kwa
mujibu wa gazeti la Daily Monitor, uamuzi huo umetolewa baada ya miezi
kadhaa ya majadiliano kati ya Mamlaka ya Kodi na Taasisi za Kidini.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.