![]() |
Mdudu tishio kwa wakulima. |
Wakulima wameeleza
hatari ya kukubwa na Baa la njaa kutokana na kuibuka kwa wadudu wanaoshambulia
zao la mahindi na maharage.
Wakizungumza na WALTER HABARI wakulima hao kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa wadudu ambao
hawafahamiki kwa majina, wamejaribu kutumia madawa mbalimbali bila mafanikio
hali inayowapa wasiwasi mkubwa wa kukosa chakula.
Wamesema wadudu hao
wanaofanana kama wale Viwa vijeshi
wanatafuna kati kati ya kiini cha mmea haswa mahindi na maharage na kuyazuia
kukua.
Walter Habari
imetembelea baadhi ya mashamba mkoani Manyara na kushuhudia mahindi yakiwa
yameharibiwa na wadudu hao.
Baadhi ya Maeneo
niliyoyatembelea ni Komoto,Daghailoy,Gadwet na Kona ya Nakwa Bagara.
Pia wakulima hao wameiomba wizara kuweza kudhibiti madawa feki ambayo hayana msaada kwao,yamekuwa yakiwapatia hasara mara nyingi.
Wizara ya
kilimo kupitia kwa afisa kilimo mkuu
Serigijuan Mtaiwa akimzungumzia mdudu
huyo amewataka wakuli ma na wataalamu wa kilimo kukagua mazao mara kwa mara.
Afisa kilimo
mkuu amesema kuwa Mdudu huyo ni mgeni hapa nchini aliingia nyanda za juu kusini mkoa wa Rukwa
katika wilaya ya Nkasi march 2017 na mpaka sasa tayari ameshaenea maeneo
mbalimbali ya Tanzania Bara.
Amesema
mdudu huyo anatokana na Nondo[Kipepeo] wanaoonekana majira ya usiku na hutaga
mayai chini ya jani ya mmea na mayai huanguliwa baada ya siku tatu na kutoa
viwavi ambavyo vinafanya uharibifu wa mazao na baadae kuwa Buu na kujichimbia
chini na kugeuka kuwa kipepeo.
Wizara imeanza
kutembelea mikoa mbalimbali na kutoa elimu kwa wataalamu wa kiulimo ili
wafikishe elimu hiyo kwa wakulima namna ya kumdhibiti mdudu huyo.
![]() |
Rangi yake ni Kijivu. |
![]() |
Akishatafuna kiini cha Muhindi anasaga na kuacha pumba pumba na pia anataga Mayai. |
Post a Comment
karibu kwa maoni