Mtoto
wa kike mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa kijiji cha Keringet kaunti
ya Pokot nchini Kenya amekutwa na sindano 7 za kushonea kwa mkono
tumboni mwake, baada ya kupigwa picha ya Xray.
Mtoto
huyo alipelekwa hospitali ya Kapenguria siku ya Jumanne kupata matibabu
ya maumivu ya tumbo ambayo alikuwa akiyapata kwa muda mrefu bila kujua
tatizo ni nini.
Bibi
yake Bi. Emily Linga'a ambaye ndiye anayeishi naye, amesema mtoto huyo
alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo kwa zaidi ya miaka miwili, lakini
hawakuweza kubaini mara moja chanzo cha maumivu hayo na kuendelea
kumpatia dawa za kutuliza maumivu, lakini baada ya kuona anazidi
kulalamika walimpeleka hospitali na kugundua ana tatizo hilo.
“Kwanza
nilidhani mtoto alikuwa na minyoo, sikuwahi kufikiria kwamba ana
sindano tumboni mwake, nilikuwa nahisi ni malaria siku zote na kumpa
dawa za maumivu”, amesema bibi huyo ambaye anaishi naye, baada ya mama
yake kumuacha alipoolewa na mwanaume mwengine.
Madaktari
wa hospitali hiyo wamempa rufaa ya kwenda hospitali kubwa ya Moi ili
kuweza kufanyiwa upasuaji wa tumbo, na kutolewa sindano hizo ambazo
hazijajulikana zimeingiaje.
Post a Comment
karibu kwa maoni