Mwanasayansi
aliyesafiri kutoka Australia mpaka Uswiss David Goodall, kwa ajili ya
kuukatisha uhai wake kesho inatarajiwa kuwa ndiyo siku ya kuhitimisha
maisha yake ya duniani baada ya madaktari kuchomeka sindano ya sumu
katika mshipa.
Kesho,
madaktari wanatarajiwa kuweka sindano iliyojazwa dawa ya sodium
pentobarbital katika mshipa wa Mwanasayansi huyo mkongwe duniani na
kumuacha aisukume mwenyewe kwenda mwilini mwake.
Goodall
amelazimika kusafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswisi kukifuata
kifo baada ya sheria za kwao kutomruhusu kufanya hivyo.
Akihojiwa
na shirika la utangazaji la Marekani CNN, Goodall amesema maisha yake
hayana thamani tena ndio maana ameamua kuomba kujiua akiamini hadithi
yake itakuwa mfano na kuhamasisha uamuzi kama huo kwa wengine waliochoka
kuishi.
Katika
mahojiano Goodall amenukuliwa akisema "Natamani ningekuwa na uwezo wa
kutembea mashambani na kuona vitu vinavyonizunguka.
"Katika umri huu naamka asubuhi, nakunywa chai. Nasubiri mchana nile halafu sina cha kufanya tena. Maisha ya aina hii ya kazi gani?
"Katika umri huu naamka asubuhi, nakunywa chai. Nasubiri mchana nile halafu sina cha kufanya tena. Maisha ya aina hii ya kazi gani?
Goodall
aliyezaliwa katika Jiji la London Aprili 1914, anatarajia kufa akiwa na
miaka 104 ambapo ameweka wazi kuwa maisha yake yalisimama miaka 10
iliyopita baada ya kupoteza uoni na uwezo wa kutembea na alitamani kama
kifo kingemchukua katika miaka hiyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni