Mchekeshaji
wa kike Bongo aliyejizolea umaarufu mpaka nje ya nchi Katarina Karatu,
amesema kauli ya Ebitoke kwamba Tanzania hakuna wachekeshaji wa kike,
amekosea kwani wako wengi sana.
Katarina
amesema licha ya kwamba hajisikii kumuongelea Ebitoke, lakini kauli
aliyoitoa haileti maana na inavunja moyo, kwani wachekeshaji wapo wengi
isipokuwa mashabiki ndio wanaamua nani ni mkali zaidi.
“Yule
ni mtu mzima anajua anachofanya kwa hiyo kuanza kumuongelea sijisikii
kwanza, nahisi sifanyi kitu sahihi, kuhusu wachekeshaji wa kike kwanza
anakosea, wapo wengi tu kuna watu wanafanya vizuri, ni mashabiki
wanaamua nani ni bora na nani anavamia fani, ila kuhusu yeye sihitaji
kumuongelea sana kwa sababu zangu binafsi”, amesema Katarina.
Mchekeshaji
huyo ameendelea kwa kusema kwamba ili kuthibitisha kuwa wachekeshaji
wazuri Tanzania wapo, hivi karibuni amepata mwaliko nchini Kenya ambapo
atapanda jukwaa moja na wachekeshaji kutoka nchi nyingine za Afrika
Mashariki, Anne Kansiime wa Uganda, Idirs Sultan wa Tanzania na wengine
wa Kenya.
Post a Comment
karibu kwa maoni