0



Mkurugenzi Mtendaji Wa Wilaya Ya Mbulu Hudgson Kamoga Amepania Kuwainua Vijana Wa Wilaya Ya Mbulu Na Mkoa Mzima Wa Manyara Kwa Ujumla Kiuchumi Kwa Kuwakutanisha Na Kuwajengea Uwezo Kwa Kuwapatia Mafunzo Ya Ujasiriamali.
Akizungumza Na Manyara Fm Na WALTER HABARI Kamoga Amesema Yeye Kama Kijana Ameamua Kuanzisha Wiki Ya Ujasiriamali,Uwajibikaji Na Uzalendo Itakayoenda Sambamba na mchezo wa mpira wa miguu pamoja na kuwapatia washiriki ambao ni vijana Mafunzo Mbalimbali ambapo  Vijana zaidi ya mia mbili Wanaojishugulisha Na Boda Boda wamethibitisha ushiriki wao.
 Ligi hiyo iliyopewa jina la KURUGENZI CUP 2018 ni UZALENDO TU,  ikiwa na kauli mbiu Ni wakati wa kuwa mzalendo na kujenga nchi yetu,Uvivu ni sumu ya Maendeleo imezinduliwa Leo May 13.2018 Katika Viwanja Vya Shule Ya Msingi Haydom Mbulu.
Kama Vijana Ni Lazima Tuwe Chachu Ya Mabadiliko Katika Maendeleo Hatuwezi Kusubiri Kila Kitu Tutegemee Kuletewa, Lazima Tutengeneze Mazingira Ya Sisi Kuwa  Wabunifu Na Kuweza Kusaidia Juhudi Za Serikali.
Aliwataka  Vijana Wa Mbulu Kuhakikisha Wanakuwa Na Vikundi Vitakavyosajiliwa Ili Iwe Rahisi Kupatiwa Asilimia Kumi 10% Ya  Ya  Mapato Ya Ndani Inayotolewa Kila Halmashauri Kwa Ajili Ya Vijana Ili Kuweza Kujikwamua  Kiuchumi.
Aliwahimiza Vijana Kujitokeza Kwa Wingi Ili Kupatiwa Semina Mbalimbali zinazotolewa,Zitakazowainua Kiuchumi Na Kuunga Mkono Juhudi Za Serikali Ya Wamu Ya Tano Inayoongozwa Na Mheshimiwa Dk.John Magufuli Katika Kufikia Uchumi Wa Kati.
Wakati Huu Sio Wa Kukaa Na Kulalamikia  Serikali Ni Muda Wa Kila Kijana Kujituma Kwa Kuongeza Bidii Katika Kazi.Alisema Kamoga.
Ligi Hiyo Imeanza Rasmi Leo May 13.2018 Na Inatarajia Kukamilika May 20 Ambapo Itafanyika Fainali Na Kufungwa Na Katibu Mkuu Wizara Ya Habari,Sanaa Na Michezo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top