Shirikisho
la Soka Tanzania(TFF) limewaondoa Waamuzi wawili kwenye orodha ya
Waamuzi wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inayoendelea kwenye vituo
vinne vya Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro.
Waamuzi
walioondolewa katika orodha hiyo ni Seleman Nonga kutoka Arusha
aliyekuwa katika kituo cha Geita na Dadu Fadhil Msemo wa Kilimanjaro
aliyekuwa kituo cha Singida.
Nonga
ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji
,kushindwa kumudu mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa
kipindi kikubwa cha mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya
Wasimamizi kwenye mchezo namba A7 kati ya Kumuyange FC dhidi ya
Ambassador.
Msemo
ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji
,kushindwa kumudu mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa
kipindi kikubwa cha mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya
Wasimamizi kwenye mchezo namba C6 kati ya Temeke Squad dhidi ya Mtwivila
City.
Waamuzi hao wawili wanatakiwa kuondoka kwenye vituo vya Geita na Singida leo Jumamosi Mei 12,2018.
TFF
haitawavumilia waamuzi watakaoendelea kuchezesha chini ya kiwango
katika mashindano hayo ya RCL pamoja na mashindano mengine yote kwakuwa
TFF imejielekeza katika uchezeshaji wa haki katika mashindano yake yote
na TFF haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayetaka kuharibu
mashindano ya RCL.
Cliford Mario Ndimbo
Ofisa Habari na Mawasiliano TFF
Post a Comment
karibu kwa maoni