0
Image result for TANZANIA PRISONS 
Ligi Kuu Tanzania Bara  inaendelea leo  na kesho, Tukianza na leo ambapo kutakuwa na  michezo miwili, Singida United FC wakiikaribisha Njombe Mji FC Uwanja wa Namfua na Tanzania Prisons FC wakiwa wenyeji wa Lipuli FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Na Jumapili Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wenyeji Maji Maji wataikaribisha Mtibwa Sugar, Kagera Sugar FC wataikaribisha Mbeya City FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Stand United FC wataikaribisha Azam FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Simba SC watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top