Wananchi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wameitikia wito kwa kujitokeza
Kusajiliwa ili wapatiwe Vitambulisho vya Taifa. Akielezea kushangazwa na
mwitiko mkubwa wa wananchi, Afisa Usajili wa NIDA wilaya ya Morogoro ambaye pia
ni Msimamizi shughuli za Usajili na Utambuzi wa watu mkoa wa Morogoro Ndg.
Sererya Wambura ameeleza kufurahishwa sana na mwitiko wa wananchi kutokana na
idadi yao kujitokeza kwa wingi tangu siku ya kwanza kwani kwa siku za nyuma idadi
ya wananchi waliokuwa wakijitokeza Kusajiliwa siku za kwanza haikuwa kubwa kutokana
na wengi kuwa na utamaduni wa kusubiri siku za mwisho ndipo wajitokeze vituoni
kwa wingi. Hadi sasa tumeshakamilisha kata 25 kati ya 29 zilizoko kwenye
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. Kata 4 zilizosalia za vijijini zoezi la
Usajili linaendeshwa kuanzia wiki hii.
Naye
Mtendaji wa Kata ya Lukobe Ndg. Moses Mangwi amewahimiza wananchi wa kata yake
ambao bado Kujitokeza Kusajiliwa, wajitokeze kwa wakati ili kuhakikisha
wanatumia fursa hiyo muhimu ili kupata haki yao ya msingi ya Kusajiliwa na
kupata Kitambulisho cha Taifa kitakachowasaidia kutambulika na kuondokana na adha
ya kutotambulika.
Aidha
Ndg. Wambura amewapa angalizo watendaji wote wa Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro kutochukua rushwa wala kutoa tozo wanapowahudumi wananchi katika zoezi
la Usajili kwani fomu ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa na huduma ya Usajili
kwa ujumla kwa mwananchi haina tozo.
Usajili
mbali na kufanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya mkoa wa Morogoro
unaendelea pia katika wilaya nyingine za mkoa huu wa Morogoro; Mvomero, Gairo,
Kilosa, Malinyi na Ulanga.
Post a Comment
karibu kwa maoni