Switzeland imeahidi
kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kusaidia Sekta mbalimbali
za Maendeleo hasa katika suala la Afya, kuongeza ajira na kukuza ujuzi .
Hayo yamebainishwa
wakati wa Mkutano Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip
Isdor Mpango na Balozi wa Switzerland hapa nchini Bi. Florence Tinguely Mattli,
ulioangazia uhusiano kati ya nchi hizo mbili na namna ya kuboresha ushirikiano.
Katika Mkutano huo
Waziri Mpango amemuomba Balozi huyo kuangalia uwezekano wa kuwapa mafunzo
madaktari Bingwa nchini ili kukidhi uhitaji uliopo hasa katika Jiji la Dodoma
ambalo ndio makao Makuu ya Nchi na idadi
ya wakazi wake inaongezeka, na pia kufadhili mafunzo kwa Watumishi wa umma ili
kuwajengea uwezo katika kada mbalimbali lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa kazi.
Aidha waziri Mpango
aliongeza kuwa miundombinu ya Jiji la Dodoma inahitaji kuboreshwa hivyo
Switzerland iangalie uwezekano wa kufadhili miradi ya maendeleo katika Sekta ya
Maji na mazingira.
“Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na mifugo
mingi Barani Afrika lakini ufugaji wa mifugo hiyo hauna ubora, kwa kuwa Switzerland
imeendelea katika Sekta ya Mifugo fursa ipo ya uwekezaji katika eneo hilo hapa
nchini” alieleza Dkt. Mpango.
Amesema kuwa
Serikali ya Tanzania inafanya jitihada mbalimbalimbali kukabiliana na umasikini
hivyo ni vema Washirika wa Maendeleo wakatambua kuwa hatua mbalimbali ambazo
Serikali inazichukua kama kupambana na wakwepa kodi na kuboresha mikataba zina
lengo la kuboresha maisha ya watanzania kwa
kuhakikisha wananufaika na rasilimali nyingi zilizopo nchini na wawekezaji waweze
kunufaika pia.
Waziri Mpango
amesema kuwa Switzerland inashiriki kikamilifu katika miradi ya Matumizi bora ya misitu hususani
Mkoani Morogoro, kuboresha ujuzi na kukuza ajira kwa Watanzania.
Kwa upande wake
Balozi wa Switzerland nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, amesema kuwa
Uhusiano kati ya Nchi yake na Tanzania umezidi kuimarika na kuahidi kuendelea
kuisaidia Tanzania katika sekta
mbalimbali za maendeleo huku akisisitiza suala la kuzingatia uwazi na mazingira bora ya uwekezaji kwa kuwa ni chachu kubwa ya kuvutia uwekezaji
wenye tija kwa pande zote mbili.
Dkt. Mpango
amemhakikishia Balozi huyo kuwa Serikali inatoa na itaendelea kutoa ushirikiano
unaohitajika katika suala la uwekezaji kwa kuwa Tanzania inaongozwa kwa utawala wa sheria unaozingatia haki.
Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara
ya Fedha na Mipango
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.