
Msako
wa kamati ya ulinzi na usalama katika maghala ya wafanyabiashara
wakubwa umebaini kuwa jijini Arusha kuna mafuta na sukari ya kutosha
hivyo ni marufuku kupandisha bei.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mei 15, 2018 baada ya msako huo jana, Mkuu
wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro amesema maghala yote ambayo
wametembelea licha ya kuwapo uzalishaji mdogo wamebaini bado kuna mafuta
na sukari.
"Kamati
ya ulinzi na usalama wilaya imetembelea maghala na kuona bado kuna
bidhaa na kwa sukari bado bei ya jumla mfuko wa kilo 50 ni kati ya
Sh102,000 na Sh110,000,” amesema.
Amesema
kutokana na bei hizo bei ya kilo moja haipaswi kuuzwa zaidi ya Sh2,600
hivyo ambao watauza zaidi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Daqarro
amesema kuhusiana na sukari iliyofungwa bei pia haipaswi kuzidi Sh2,800
na taratibu zinafanywa kuhakikisha bei haiongezeki.
Kuhusiana na mafuta pia amesema yapo ya kutosha ikiwapo ya alizeti licha ya uzalishaji kupungua.
Baadhi
ya wakazi wa Arusha waliomba Serikali kuendelea kudhibiti kupanda bei
ya mafuta na sukari hasa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Jasmin Ally mkazi wa makao mapya amesema katika maduka mengi kati kati ya jiji sukari inauzwa kilo kati ya Sh2,700 na Sh2,800.
Hillal Kusena amesema bei ya mafuta na sukari inaendelea kupanda licha ya matamko ya Serikali.
"Serikali ingefatilia kujua tatizo ni nini kama ni kodi kubwa basi wapunguze lakini kutoa matamko tu hakutoshi," amesema Kusena.
Amesema
bei ya mafuta ya kupikia bei ya jumla imepanda kutoka Sh 61,000 hadi Sh
70,000 kwa lita 20 huku lita 10 imepanda kutoka Sh 30,000 hadi
Sh35,000.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.