0

Image may contain: 10 people, people smiling, outdoor
Kikosi cha Timu ya Usalama Sc,Bingwa kutoka Babati Manyara.

Ligi ya mabingwa wa mikoa imeanza kutimua vumbi leo jumapili  mei 6.2018 katika viwanja mbalimbali ambapo kwa Kilimanjaro mchezo Kwa kituo cha Kilimanjaro  mamia ya mashabiki wa mkoa huo na jirani zake Arusha na Manyara walikuwa wakishuhudia Kabumbu likitandazwa.

Katika uwanja wa Boma Hai Kilimanjaro walikutana watoto Uzunguni kutoka Boma Hai wakifundishana mpira na washika Bunduki wa Babati,Usalama Sc ya Manyara huku watoto wa Uzunguni wakionekana kuzidiwa nguvu mapema na wababe hao kutoka mji wa Mbaazi Babati.

Magoli ya usalama yamefungwa na Majaliwa Juma dk ya 29,akarudi tena dk ya 43 na kupachika la pili wakati bao la tatu limewekwa kimiani na Said Chandona dk ya 80.

Uzunguni walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 3 ya mchezo kupitia  kwa mchezaji wao Ramadhani Juma.

Ligi hiyo ya RCL inashirikisha timu 28 zilizogawanywa kwenye makundi manne kwenye vituo vya Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro na kila kundi kwenye kituo likiwa na timu 7.

Kila kundi litapandisha timu 2 wakati zitakazobaki zitarudi ligi ya mkoa.
Ligi hiyo inatarajiwa kukamilika mei 22.2018.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top