Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema jalada la uchunguzi
wa watu wanaosambaza vitabu mitandaoni limefunguliwa.
Akizungumza
jana Ijumaa Mei 4, 2018 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Kamanda
Sirro amesema wamepokea maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.
"Tumepokea maelekezo na tayari tumefungua jalada na tutakapowapata tutawapeleka mahakamani," alisema IGP Sirro.
Kuhusu
watu wanaovunja sheria ya mitandao, IGP Sirro amesema wanaendelea
kufuatilia na kila atakayekuwa anabainika wanachukuliwa hatua kwa mujibu
wa sheria.
Post a Comment
karibu kwa maoni