TAMASHA la Notting Hill jijini London limetiwa doa kutokana na kuuawa kwa rapa chipukizi na maelfu ya watu kukamatwa, Polisi wamesema jana Jumanne.
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 21 alifariki baada ya kuchomwa kisu Jumatatu, hilo likiwa ni tukio jipya katika wimbi la matukio ya uhalifu wa kutumia kisu katika mji huo mkuu wa Uingereza mwaka huu na kusababisha wasiwasi.
Rapa huyo aliyeuawa alijulikana baadaye kuwa anatokea Bristol, magharibi mwa England, na ambaye alikuwa akitumia jina la TKorStretch.
“Alikuja kutoka Bristol ili kuburudika tu katika tamasha la London na haya ndio matokeo yake,” meneja wake, Chris Patrick aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.
“TK alikuwa kijana mzuri, mtu mzuri na kilichotokea kimeumiza moyo wangu,” aliongeza.
Polisi wa London wamesema maofisa wake walipigiwa simu saa 2:00 jioni Jumatatu, siku ya mwisho ya tamasha, kupewa taarifa za tukio la kuchomwa kisu lililotokea Ladbroke Grove na waksimamia huduma ya kwanza.
“Alipelekwa hospitali iliyoko magharibi mwa London, ambako, licha ya juhudi za madaktari, alitangazwa kuwa amefariki.
Post a Comment
karibu kwa maoni