Na John
Walter
Babati-Manyara
Wakati dunia
imetoka kuazimisha siku ya kina Mama duniani May 14 ikifuatiwa na siku ya
Familia May 15 bado vitendo vya kina Mama kunyanyasika na Familia kuvunjika
vinaonekana katika jamii nyingi hapa nchini.
Siku ya Familia
mwandishi wa Habari John Walter anaefanya kipindi cha mtaa kwa mtaa 92.1 Redio Manyara
fm alitembelea baadhi ya Familia ili kujua namna wanavyosheherekea
siku hiyo na kukutana na Mwanamama mmoja aliesimulia magumu yanaisibu Familia
yake.
Katika mitaa
niliyotembelea ni apmoja na Gendi uliopo mjini Babati mkoa wa Manyara ambapo
alichokikuta ni tofauti alivyotarajia katika moja ya Familia huko Gendi.
Wengi
wamezoea kusikia Mama akitoroka nyumbani na watoto na kuacha Nyumba lakini hii
imekuwa tofauti kidogo kwenye Familia ya Sebastian Blass na Bi Magdalena Joseph
ambapo Baba ndie aliechukua uamuzi wa kutoroka na watoto wake wawili aliewazaa
yeye pamoja na bi Magdalena.
Bi Magdalena
anasema kuwa akiwa na mwanaume huyo wamefanikiwa kupata watoto wane ambao
wawili walipoteza Maisha na kubakiwa na wawili mmoja wa kiume na mwingine wa
Kike ambao wote mwanaume ameondoka nao na kwenda kusikojulikana.
Akielezea
kisa hicho mwanamke huyo amesema awali walikuwa wakiishi kwa upendo na amani
lakini mara baada ya mwanaume huyo kutoka safarini ndipo akaanza kumfanyia visa
mbalimbali huku akimwambia kuwa hamtaki aondoke na awaache watoto.
Hatua
aliyoichukua mwanamke huyo alifika katika ofisi za mtaa ambapo alipatiwa barua
iliyomwelekeza kwenda kituo cha polisi.
Baada ya
kufika kituo cha Polisi Dawati la jinsia na watoto mjini Babati alipatiwa barua
nyingine ya wito ikimtaka mwanaume kuripoti katika kituo cha polisi lakini
hakufanikiwa kumpata mwanaume huyo kwani tayarai alishaondoka.
Mkaguzi
msaidizi wa jeshi la Polisi kutoka dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Manyara
Afande Pili Pilo alipozungumza na kipindi hiki kwa njia ya simu alionyesha
kusikitishwa na kitendo hicho akielekeza kuwa mwanamke huyo atoe ushirikiano
ili mwanaume huyo asakwe popote alipo na kufanyiwa mahojiano.
Nao majirani
wameeleza kuwa wameshangazwa na kitendo cha mwanaume huyo kumtelekeza mwanamke
wake na kwamba amemdhalilisha mwanamke wake pamoja na wanaume kwa ujumla kwa
kitendo hicho ambacho sio cha kibinadamu.
Wengine
wameeleza kuwa hiki ndio chanzo cha kuwepo kwa watoto wa mitaani ambao baadae
yanazaliwa makundi mbalimbali ya wahalifu.
Mkoa wa
Manyara ni moja kati amikoa yenye vitendo vini vya ukatili kwa wanawake na
watoto haswa ukeketaji.
Post a Comment
karibu kwa maoni