0


 
Watu wawili wamepoteza maisha katika ajali iliyosababishwa na trekta  katika kijiji cha Terrati wilayani Simanjiro Mkoani Manyara na kusababisha majeruhi 45 kati ya watu 50 ambapo trekta hilo lilipoteza mwelekeo na kupinduka.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 3 asubuhi Kamishna Msaidizi wa jeshi la Polisi Mkoani Manyara ACP  Issa Bukuku alifafanua kwa kusema kuwa  Trekta hilo lilipakia watu kupita kiasi   wakielekea kwenye tamasha la uimbaji katika kanisa la kiinjili la kilutheri.

Aliwataja marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Paulina Matuna (50) na Nasiganda Sakuta (15)wote wakazi wa Simanjiro,Bukuku alitoa wito na kuwata wananchi kutokupakia abiria katika vyombo vya moto ambavyo haviruhusiwi kisheria ili kuepuka ajali.

Katika matukio mengine Kamishna Bukuku alisema mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Nkaiti wilayani Babati aliyetambuliwa kwa jina Kaiyai Letete (40)na Paulo Leitete (33)wamekamatwa na nyara za Serikali Nyama ya Pundamilia ambayo hairuhusiwi kisheria watu hao wanashikiliwa na jeshi la polisi.

Katika tukio lingine lilitokea tarehe 4 juni mwaka huu katika eneo la Minjingu  mkazi wa Babati Mkoani hapa Rajabu Msafiri maarufu Samwel (17) amekamatwa na Mabunda 40 ya mirungi katika basi liitwalo Capricon lenye nambari za usajili T 133 AUJ. likitokea Moshi kulekea  Singida.
Aliongeza kuwa katika tukio lingine lilitokea juni 3 mwaka huu mkazi  wa Galapo wilayani Babati Fatuma

Athumani (45) amekamatwa na misokoto 1130 ya bangi katika eneo la Minjingu katika basi la kampuni ya Capricon lenye nambari za usajili T 280 BQJ likitokea Same kuelekea Singida

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top