0

Image result for CCM
Uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa ccm  Babati vijijini umefanyika baada ya kuwa umeaahirishwa siku ya ijumaa kutokana na sababu mbalimbali huku mgombea alieshindwa akikiri  kuwa alitoa rushwa.
Katika uchaguzi huo wagombea walikuwa wawili baada ya mmoja kujitoa na baada ya kura zote kuhesabiwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Martha Umbura akatangaza matokeo ambapo  Gabriel  alipata kura Lusian 378,na Abdilahi  Sogora akatangazwa kuwa mwenyekiti kwa kupata kura  399.
Aliyechaguliwa sasa  alikuwa akitetea nafasi yake hivyo ataongoza tena kwa miaka mingine mitano na kufanya muda aliongoza madarakani kufikia miaka 20.
Katibu wa ccm wilaya ya Babati vijiijini anaeleza kuwa hakuna mgombea aliekamatwa na rushwa na kwamba chama hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti Rais John Pombe Magufuli kinapiga vita vitendo vya Rushwa.
Aidha katibu amesema kuwa chama kwa sasa kimejipanga kubadilisha mfumo katika kutoa majina ya wagombea katika chaguzi zinazokuja kuanzia ngazi ya serikali za mitaa mpaka uchaguzi mkuu  ili kuepuka vitendo vyovyote vya ushawishi kwa wapiga kura.
Uchaguzi wa mwaka huu tumeshuhudia viongozi wanaoshindwa kulalamika na kusema rushwa imetumika katika kushawishi wajumbe.
Katibu wa Ccm Babati vijijini Edna Edmund Khera amekiri kuwa Rushwa Na ukanda ni mambo ambayo yamegubika kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi wa mwaka huu na kuwataka wanachama wanapohisi vitendo vya rushwa watoe taarifa mapema au wapekeke ushahidi.
Mwenyekiti aliechaguliwa Abdilahi Sogora akawashukuru zuyngumza haya huku akiwashukuru wanachama kwa kumchagua tena.
Uchaguzi wa chama cha Mapinduzi ngazi ya wilaya umekamilika na kwa sasa unaofuata ni chaguzi katika ngazi ya mkoa mwezi novemba mwaka huu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top