0


Image result for MASANGE KONDOA 
Sakata la kudai taarifa ya mapato na matumizi katika kijiji cha Kwayondo kata ya Masange wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma baada ya kuripotiwa na Manyara FM sasa imengia katika Sura nyingine baada ya wajumbe kugoma kuhudhuria mkutano mkuu wa kijiji ulioitishwa kijijini hapo.

Awali Wakazi wa kijiji cha kwa Yondu kata ya Masange  waliulalamikia uongozi wa kijiji hicho  kupitia redio MANYARA FM na WALTER HABARI,kushindwa kusoma taarifa ya mapato na Matumizi kijijini hapo kwa takribani miaka saba sasa hali inayowapa mashaka kuwa fedha wanazozichanga kwa ajili ya Maendeleo ya kijiji zinatafunwa na wajanja wachache.

Wameuambia mtandao wa WALTER HABARI kuwa hawana Imani na viongozi wa kjiji hicho haswa Mwenyekiti na Afisa mtendaji.

 Mwenyekiti wa kijiji hicho Khalifa Abubakar licha ya kukiri kuwa hawakusoma mapato na matumizi kwa wanakijiji kwa miaka saba, alipoulizwa na mtandao huu kuhusu tuhuma hizo alisema anashangaa taarifa hizo kufika katika vyombo vya habari.
Ameongeza kwa kueleza kuwa tuhuma hizo hazimhusu kwani hakuwepo katika miaka hiyo saba.
 
Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho Mohamedi Iddy Nkechu amesema kikao hicho ni mara ya 12 sasa kinagomewa na wanakijiji.

Afisa Mtendaji wa kata ya Masange Fatina Ramadhani akijibu kuhusu hilo alidai kuwa taarifa hizo sio za kweli.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top