0
Dk Tulia Ackson Mwansasu amempeleka Mbunge wa Iringa  Mch Peter Msigwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili akatoe ushahidi wake wa namna ufisadi ulivyofanyika kwenye mradi wa mfumo wa uhamiaji mtandao (E-Immigration)

Tulia Ackson amesema hayo baada ya Msigwa kudai kuwa ana taarifa za kutosha juu ya ufisadi uliofanyika katika mradi uliozinduliwa na Rais Magufuli hivi karibuni na kudai kuwa Kambi ya Upinzani bungeni wanazo nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka kuhusu namna ufisadi ulivyofanyika katika mradi huo chini ya Serikali ambayo inajipambanua kupambana na ufisadi. Kufuatia kauli hiyo ndipo hapo Naibu Spika aliagiza Mbunge huyo kwenda kutoa taarifa hizo kwa Kamati ya maadili. 

"Mhe. Msigwa taarifa ulizonazo kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye hili zoezi zipelekwe kwenye hii kamati, Kamati itakuja kulishauri bunge tufanye nini na huo ufisadi unaoendelea hayo maeneo kwa hiyo naiagiza kamati imuite Mhe. Peter Msigwa na yeye namuagiza Mhe. Msigwa apeleke huko hizo nyaraka ili bunge liweze kushauriwa na kuchukua hatua mahususi" alisema Tulia Ackson.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli  Januari 31, 2018  alizindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top