Umoja wa
wanawake Tanzania [CCM] mkoa wa Manyara umeguswa na watoto yatima wanaosoma
shule ya msingi ya serikali Bonga Halmashauri ya mji wa Babati na kuamua
kujitolea kuwanunulia sare za shule na Viatu.
Februari
3.2018 Umoja wa wanawake waliwatembelea wanafunzi hao katika shule hiyo ikiwa
ni katika kusheherekea miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi ambapo
waliguswa na watoto hao hali iliyowalazimu kurudi tena baada ya kukubaliana
pamoja na wabunge wa viti maalum wa Ccm Ester Mahawe na Martha Umbura kuwa
wawasaidie wanafunzi hao.
Kwa mujibu
wa Katibu wa Umoja wa wanawake mkoa wa Manyara Hainess Munis ameeleza kuwa Wabunge
hao kwa pamoja wamekubaliana kuwasaidia watoto hao kwa kuwapatia sare za
shule, viatu na mahitaji mengine.
Watoto hao
ambao wameondokewa na wazazi wao wamefarijika kuona jamii ipo karibu nao na
kuonekana wakitabasamu.
Mkuu wa
shule ya msingi Bonga January Barnabas anasema kuwa kuna jumla ya watoto 37
ambao ni yatima na uwezo wao darasani unaridhisha.
Aidha mkuu
huyo amewapongeza wanawake wa umoja wa wanawake wa Ccm Manyara pamoja na
wabunge wa viti maalum kwa msaada walioutoa na kuwataka wengine waige mfano huo
wa kuwapa msaa hata pindi wanapohitimu elimu ya msingi waweze kuendelea mbele
zaidi.
Katika hatua
nyingine Chama cha mapinduzi kupitia jumuiya ya wanawake UWT MANYARA
Wamemsaidia mtoto Angelina Lucas mwenye miaka 14 mwanafunzi wa darasa la tano
shule ya msingi Katesh anayesumbuliwa na tatizo la Macho na miguu kwa kumkatia
bima ya afya na kumfungulia akaunti Benki.
Bibi wa
mtoto huyo Hadija Shabani anasema ameahangaika kwa muda mrefu kutafuta pesa za
matibabu ila kupitia bima waliopatiwa na Ccm anaamini mjukuu wake atapona.
Post a Comment
karibu kwa maoni