
Kupitia mahubiri Yake yaliyorushwa na kituo cha redio cha Amazing Grace, Niyibikora alisema kuwa wanawake hawapendwi na Mungu huku akionya kuwa “hakuna lolote jema linaloweza kupatikana kutoka kwa Wanawake”.
”Unaposoma Biblia , ni nani aliyeleta dhambi duniani”? Aliuliza akiongeze, ”sio mwanamume”, alisema muhubiri huyo.
Kwa mujibu wa gazeti la New Times linasema kuwa mahubiri hayo yamewakasirisha wanaharakati huku wale wanaounga mkono usawa wa kijinsia wakiitisha mkutano na vyombo vya habari na kuonya kuwa maneno kama hayo yanaweza kusababisha chuki na mzozo miongoni mwa raia wa Rwanda iwapo hakuna hatua ya haraka itachukuliwa.
Kutokana na mahubiri hayo kukasirisha wengi kanisa la Seventh Day limefanya juhudi za kujitenga na Niyibikora ambaye wanadai alipigwa marufuku kwa miaka mitano iliyopita.
Post a Comment
karibu kwa maoni