0
Wanajeshi zaidi ya 250 wanaripotiwa kufariki dunia baada ya ajali ya ndege ya kijeshi kutokea asubuhi ya leo April 11, 2018 huko nchini Algeria.
Ajali hiyo imetokea muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Boufarik karibu na Mji Mkuu wa Algiers, lakini mpaka sasa sababu za ajali hiyo bado hazijajulikana.
Video za CCTV zimeonesha eneo hilo limefunikwa na moshi mkubwa huku taarifa zikieleza kuwa magari ya wagonjwa 14 yamefika katika eneo la tukio kutoa msaada.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top