Mwanafunzi
wa darasa la nne katika shule ya msingi Sabasaba jijini Mwanza, Dotto
Baraka (13) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri ya simu
aliyokuwa akiiunganisha na radio chakavu.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo ambapo
amesema limetokea Mei 17, mtaa wa Igoma Mashariki jijini Mwanza.
“Baada
ya kutoka shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza kutengeneza
radio chakavu kwa kuchukua betri ya simu na kuunganisha kwenye nyanya
za radio hiyo akitumia mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na kusababisha
kifo chake," amesema Kamanda Msangi.
Aidha
Kamanda Msangi ameongeza kuwa wakati tukio hilo linatokea, wazazi wa
watoto hao walikuwa safarini huko wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Hata
hivyo katika tukio hilo hakuna mtoto mwingine aliyejeruhiwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni