0
Responsive imageMgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Kiteto iliyoko mkoa wa Manyara na Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga uliodumu kwa miaka 20 na kusababisha mauaji ya watu zaidi ya 150 na uharibifu wa mali za wananchi hatimaye umepatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Akizungumzia kuhusu mgogoro huo katika mkutano wa hadhara mpakani mwa Wilaya za Kilindi na Kiteto,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  amesema wataalamu wa ardhi waliotumwa na wizara kufanya uhakiki wa mpaka huo, ndio waliosababisha kuwepo kwa mgogoro kwa miaka mingi kutokana na kujihusisha na rushwa na kusababisha upimaji kufanyika kwa upendeleo.
Ufumbuzi umeweza kupatikana baada ya wataalam wa ardhi na ramani kufanya kazi ya uhakiki wa mpaka kupitia maelekezo ya waziri mkuu yaliyotaka mipaka yote iliyohakikiwa miaka ya hivi karibuni ifutwe.
Naye Mbunge wa Kiteto  Emmanuel Papian amewataka wananchi hao kuheshimu maamuzi yanayotolewa na serikali ili kuepusha migogoro ambayo haina tija kwa taifa.
Walter habari inaomba Serikali kupitia idara zinazohusika iwe makini katika kupima maeneo mapema na kuweka mipaka itakayobainisha mpaka kwa mpaka ili kuepuka migogoro inayopelekea watu wasio n hatia kupoteza maisha.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top