0
Jeshi la polisi mkoani Manyara limesema kuwa limeendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu na biashara ya madawa ya kulevya kwa kufanya doria zake usiku na mchana.
Akizungumza na Manyara Fm ofisini kwake leo kamishna msaidizi wa  jeshi la polisi mkoa wa Manyara Longinus Tibishubwamu ameeleza kuwa kwa  kipindi cha mwezi mmoja hawajapata tukio lolote la uhalifu na kwamba jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi linaendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu.
Akizungumzia hali ya usalama bara barani amesema kuwa madereva boda boda wanaongoza kwa kuto tii sheria za bara barani kwa kutovaa kofia ngumu,kubeba abiria zaidi ya mmoja [mishikaki] licha ya kupatiwa elimu mara kwa mara na jeshi hilo.
Hata hivyo Tibishobwamu amewataka wakazi wa Manyara kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili mkoa uendelee kubaki katika hali ya usalama.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top