Viongozi wa
Dini nchini, wamesema Rais John Pombe Magufuli hajakataa kuonana na kuzungumza
nao kama inavyoelezwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya
habari.
Hayo yamesemwa jana na Sheikh Mkuu wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum ambapo alikanusha taarifazilizochapishwa na gazeti la
Tanzania Daima la Septemba 21 ISSN 0856 9762 toleo namba 4310 na kusema kwamba
taarifa hizo sio za kweli na zina nia ya kuchonganisha wananchi na viongozi wa
dini na Rais Magufuli.
Na kuwaonya
wasifanye hivyo, kwani Taifa ni letu sote. Aidha, Sheikh Mkuu ameeleza bayana
kuwa nia ya viongozi hao kutaka kukutana na kuzungumza na Rais Magufuli ni
kutokana na maono yao waliyoyapata kutoka kwa Mungu na sio kwamba wameagizwa na
UKAWA.
Amesema kuwa
tayari wameandika barua kwenda kwa Rais Magufuli ikiwa imesainiwa na Katibu
Mkuu wa BAKWATA, Katibu Mkuu wa TEC na Katibu Mkuu wa CCT hivyo wanaamini kuwa
Rais Magufuli ataafiki ombi lao.
Ameeleza kuwa Rais Magufuli ni Rais makini,
anawaheshimu viongozi wa Dini ndio maana kila mara huomba wananchi na viongozi
wa dini wamuombee aweze kutekeleza majukumu yake.
Hivyo amewasisitiza wananchi kupuuza uvumi wa
aina yoyote unaoenezwa kuhusu mkutano wao na Rais.
Post a Comment
karibu kwa maoni