Zaidi ya makokoro 90 yenye thamani ya Shilingi Milioni 56.4
yaliyokamatwa yakitumiwa na wavuvi haramu katika Ziwa MANYARA na BURUNGE
Mkoani MANYARA yameteketezwa kwa moto na wahusika kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria.
Mkuu wa Mkoa wa MANYARA, JOEL BENDERA ameagiza watu watakaokamatwa na
nyezo haramu za kuvulia samaki ama samaki waliovuliwa kinyume cha
sheria mali zao yakiwemo magari na pikipiki zitaifishwe.
Awali katika maelezo yao Mkuu wa Wilaya ya BABATI Mhandisi RAYMOND
MUSHI na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, HAMIS MALINGA wamesema
uvuvi unaofanyika katika maziwa hayo si endelevu.
Post a Comment
karibu kwa maoni