ZAIDI ya Wanafunzi elfu kumi wa shule za msingi mkoani MANYARA walionza
Darasa la kwanza mwaka 2010 hawajamaliza shule kutokana na sababu mbali
mbali zikiwemo za utoro, mimba, magonjwa na vifo.
Kaimu Afisa Elimu wa mkoa wa MANYARA LAGO SILLO amesema idadi hiyo
ni sawa na asilimia 28.33 ya Wanafunzi 36,611 walioandikishwa darasa la
kwanza mwaka 2010, ambapo kati yao wanafunzi 26,239 ndio waliosajiliwa
kufanya mtihani wa kumaliza Darasa la saba mwaka huu sawa na asilimia
71.67.
Katika taarifa yake wakati wa mkutano wa kuchagua Wanafunzi wa
kujiunga na kitato cha kwanza mwaka ujao, Kaimu Afisa Elimu wa mkoa wa
MANYARA ,LAGO SILLO amesema mkoa unahitaji nguvu ya pamoja ya kupunguza
mdondoko wa Wanafunzi shuleni.
SILLO mkoa wa MANYARA umeshuka kutoka nafasi ya 19 kitaifa mwaka jana
katika matokeo ya darasa la saba na kuwa mkoa wa 20 mwaka huu, licha
kuwa ufaulu umeongezeka kutoa asilimia 59.18 mwaka jana hadi kufikia
asilimia 62.60 mwaka huu.
Post a Comment
karibu kwa maoni