0

Saidi Mohammed anaetuhumiwa kumnyanyasa Mtoto wake wa kumzaa mara baada ya mama yake kufariki na kuoa wake wengine wawili Mtaa wa Nangara Ziwani Babati mjini.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka sita afya yake imedhoofu na kumpelekea kupata kiriba tumbo.
Jeshi la polisi Mkoani Manyara kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto linamshikilia Baba wa mtoto huyo.
Majirani, wasamaria wema wanasema wanapohitaji kumsaidia anawafukuza kwa kutumia silaha za jadi.
Hilo limegundulika wakati Jeshi la polisi nchini lipo katika kupinga Ukatili wa watoto na wakina mama kwa siku 16.
kauli mbiu ya mwaka huu FUNGUKA PINGA UKATILI WA KIJINSIA ELIMU SAWA KWA WOTE. 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top