Leo May 24,
Ikulu Dar es salaam Rais Magufuli amepokea ripoti ya Kamati Maalum iliyoteuliwa
na Rais kuchunguza mchanga wa madini kwenye makontena 277 yaliyozuiwa na
serikali kusafirishwa kwenda nje kwaajili ya uchenjuaji.
Kamati hiyo
iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Mruma imemkabidhi ripoti iliyoonesha kuna
upotevu mkubwa wa mapato na rasilimali za nchi, ambapo ripoti imesema Tanzania
inapoteza kiasi cha Tsh. Bilioni 829.4 hadi Trilioni 1.439 kwa kusafirisha
mchanga nje ya nchi.
Prof. Mruma
ametoa mapendekezo ya kamati hiyo kuwa kama ifuatavyo.
Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga mpaka
mrabaha stahiki utakapolipwa kwa kuzingatia thamani halisi ya makinikia.
Tepe za udhibiti zifungwe mara moja ili kuepuka
udanganyifu unaoweza kufanyika wakati wa kuchukua sampuli.
TMAA ipime metali zote zilizomo kwenye makenikia
ili kupata thamani halisi ya metali hizo( mrahaba).
Kutokana na uwepo wa madini kwenye mbale, TMAA
ipime viwango vya metali zote muhimu ktk mbale bila kujali nyaraka za
msafirishaji.
Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na
wale wa wizara husika.
Pamoja na vyombo vya uhakiki, Serikali iweke mfumo
wa kushtukiza ili kuepuka watendaji kufanya kazi kwa mazoea.
Serikali itumie wataalamu wa mionzi ili kufunga
scanner zenye uwezo sahihi kwa ajili ya makinikia na mizigo mingine.
Ujenzi wa vinu vya uchakataji ufanyike haraka ili
madini yote yaweze kufahamika na kutozwa mrabaha sahihi..
Uchunguzi zaidi ufanywe na wataalam wa mionzi
kwenye scanner zinazotumika bandarini ili kubaini aina au mfumo sahihi wa
scanner unaofaa.
Post a Comment
karibu kwa maoni