
Watuhumiwa wa ugaidi wanaoshikiliwa katika magereza
jijini Arusha jana wametishia kugoma kufika tena mahakamani kwa ajili ya
kusikiliza kesi zao, wakidai kuwa upelelezi wa kesi yao umechukua muda mrefu.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Azam TV,
watuhumiwa hao waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini
Arusha, wameiambia Mahakama hiyo kuwa huenda wakagoma kufika mahakamani hapo
endapo kesi zao hazitaanza kusikilizwa.
Hata hivyo, Hakimu wa Mahakama hiyo aliwataka
watuhumiwa hao kuendelea kufika mahakamani kama kawaida kwani mashauri yao
yanaendelea kushughulikiwa. Aliwataka kufika Mahakamani ili waweze kufahamu
mwenendo wa kesi zao.
Watuhumiwa hao walikamatwa kwa makosa ya ugaidi
takribani miaka minne iliyopita na kupandishwa kizimbani. Upande wa Jamhuri
unaendelea kukamilisha upelelezi wa mashtaka yao.
Post a Comment
karibu kwa maoni