
Baada
ya kusikiliza maoni ya baraza la wazee leo Mahakama kuu ya tanzania,
imesema Elizabeth Michael amekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia,
muigizaji mwenzake Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake na hukumu
yake itatolewa Novemba 13.
Wazee
hao ambao walikuwa watatu, kila mmoja alitoa maoni yake na kusema
kwamba muigizaji huyo ana hatia ya kuua bila kukusudia, kwani marehemu
alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya mshtakiwa.
Kabla
ya wazee kutoa maoni, Jaji Rumanyika ambaye ndiye anayeendesha kesi
hiyo, alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kusema kwamba
ushahidi upande wa mashtaka umejikita katika ushahidi wa kimazingira kwa
kuwa Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba, kisha kusikiliza maoni
hayo.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 13, ambapo hukumu yake itasomwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni