Anaandika Veronica Kazimoto kutoka Dar es Salaam.
Maadhimisho ya Siku ya Takwimu
Afrika yanafanyika leo tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi wa
Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya alisema
maadhimisho hayo yanayoratibiwa na ofisi hiyo kwa niaba ya Serikali, yana lengo
la kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa Tasnia ya Takwimu katika kuleta
maendeleo ya kiuchumi na kijamii Barani Afrika.
Ruyobya alisema kuwa kaulimbiu
ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha
Bora"
"Kaulimbiu hii inalenga
kuweka mkazo katika matumizi ya Takwimu za Uchumi kwa ajili ya kuboresha maisha
ya wananchi wote nchini na Afrika kwa
ujumla", amebainisha Ruyobya.
Ruyobya alifafanua kuwa
matumizi sahihi ya Takwimu za Uchumi yanaiwezesha Serikali kutunga sera na
kutathmini programu mbalimbali kama vile Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka
Mitano (FYDP-II), Agenda ya Dunia ya Mwaka 2030 ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) na Agenda ya Afrika ya Mwaka 2063.
"Progaramu zote hizi, zina
lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhakikisha kuwa, kuna upatikanaji wa
Huduma za afya, Elimu, Miundombinu ya umeme na barabara, Mawasiliano, Utunzaji
wa mazingira pamoja na Utawala bora", amesema Ruyobya.
Jumla ya washiriki 200 kutoka
katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Vyuo vya Elimu
ya Juu, Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Wadau mbalimbali wa takwimu
nchini wanatarajiwa kuhudhuria kwenye maadhimisho hayo.
Siku ya Takwimu Afrika
huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Novemba ambapo kwa mwaka huu, Tanzania
itaadhimisha siku hiyo kesho tarehe 20 Novemba, 2017.
Post a Comment
karibu kwa maoni