0
Msanii wa Bongo Fleva Beka Fleva anaetamba kwa sasa na kibao chake "SIKINAI" amewaambia mashabiki wake kuwa  wajiandae kupokea vitu vizuri zaidi mwaka 2018.
Beka Fleva akizungumza na Manyara Fm pia amezungumzia  ishu ya Aslay kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja akisema kuwa ni mfumo wake aliojiwekea na ni kitu kizuri.
Kuhusu maneno ya kwenye  mitandao ya kijamii  kwamba Aslay katoroka na daftari la nyimbo amesema huo ni uzushi wa mitandao ya kijamii 'Mbona hata mimi nina Counter'.
Pia Beka amesema yeye hawezi kutoka kwa msichana ambaye amemzidi umri.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top