0
Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Mheshimiwa Jitu [CCM] katika msimu huu siku kuu amewataka watanzania kusheherekea kwa kuwatembelea watu wenye shida mbalimbali.
Mheshimiwa Jitu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wazee katika kituo cha kulelea wazee wasiojiweza Kijiji cha Sarame kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara akiwa ameambatana na watangazaji na waandishi wa habari wa redio Manyara waliofika katika kituo hicho kuwapelekea misaada mbalimbali ya mavazi na chakula pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Katika ziara hiyo Maalum Jitu aliupongeza uongozi wa 92.1 Mfm kwa kuandaa ziara hiyo ambayo imewapa faraja wazee na kujisikia wenye furaha.
Aidha Jitu ameahidi kuwapatia wazee redio pamoja na King'amuzi ili waweze kusikiliza na kutazama taarifa mbalimbali na burudani.
Awali kituo hicho kilikuwa kikikabiliwa na tatizo la usafiri kwa ajili ya kuwapeleka wazee hao katika kituo cha afya pindi walipokuwa wakiugua lakini kwa sasa kwa uongozi wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli umekipatia kituo Bajaji hatua iliyopongezwa na wazee pamoja na viongozi wanaowasimamia.
Pamoja na hayo amesema kuwa kwa sasa anaendelea kuwajibika kwa wananchi wake wa jimbo la Babati vijijini  waliomchagua kuwa Mbunge kwa kuwaletea maendeleo bila kuangali itikadi za vyama vyao.
MSIKILIZE HAPO CHINI

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top