Na Gharib
Mzinga.
Hakuna shaka
kitu kizuri hupendwa na wengi, lakini hakipendwi na wote.
katika
kandanda kuna suala liitwalo ushabiki, ni kitu kizuri sana kuwepo, ushabiki
unaleta radha kamili na maana nzima ya soka.
Ushabiki huu
unapelekea watu kuamua kuukataa ukweli hata ukiwa upo wazi.
Hakuna haja
ya ubishi, Tukiweka ushabiki kando Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib ni
miongoni mwa wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa sana katika ligi kuu Tanzania
Bara.
Hauitajiki
kua mshabiki wa Yanga ili kukubali hili.
Ajib ni
mshambuliaji aliyelelewa katika kikosi cha vijana cha simba sc, kabla
hajapandishwa kikosi cha kwanza na baadae kutimkia Katika Club ya Yanga sc,
ambayo ni hasimu mkubwa wa simba, kwa ada ya shilingi milioni 50 za kitanzania,
alijiunga huko baada ya simba kushindwana nae kimaslahi.
Kitendo cha
Ajib kujiunga na Yanga kiliwakera sana wanamsimbazi, Hali iliyopelekea Ajib
asemwe sana kwa kauli mbali mbali zikiwemo, msaliti, mbinafsi, alikua ana
mapenzi na yanga kila aina ya mabezo alipatiwa.
Simba
wakajibu mapigo kwa kumsajili Kiungo mashuhuri wa Yanga Haruna Niyonzima.
Ibrahim Ajib
amekua akisemwa kwamba ni Mvivu, Mtegezi, Hapendi kukaba na hafanyi mazoezi ya kutosha
ndio maana alipokua na Simba hakua akimaliza dakika 90.
Kauli hizi
zimeandikwa na kusemwa na wadau wengi wa soka wanaomfaham vizuri Ajib.
Kutokana na
kudharauliwa, kuitwa garasa kutukanwa na kubezwa kwa hali ya juu, Ibrahim Ajib alipojiunga
na Yanga aliamua kuwaonesha watu wanaomsema vibaya hususan washabiki wa klabu yake
ya zamani kua yeye ana uwezo mkubwa na wamefanya makosa kumuacha.
Katika
michezo Ya Awali ya ligi kuu tanzani Bara, Ibrahim ajib alicheza katika kiwango
cha juu sana, akawa anafunga, anasaidia mabao mengi, hatari katika mipira ya
kufa, ukitaka kuamini hilo kaangalie rekodi ya michezo sita ya mwanzo ya yanga,
alizinyanyasa timu kama vile Lipuli, Njombe mji, majimaji,ndanda mtibwa na
kagera sugar.
Ibrahim Ajib
ambaye watu wengi walikua wakimtaka ndiye Yule wa michezo ile sita ya Awali, alifanya
kila jambo uwanjani, Aliibeba yanga katika mabega yake, alifanya hivyo kwa
kusudio la kuwaonesha simba kua Ajib ni nani, hata katika mchezo dhidi ya
Kagera akaamua kuwaonesha wapinzani jina lake na namba ya jezi yake kama
alivyofanya Leonel Messi, Cristiano Ronaldo na Mauro Icard.
Lait kama
kile kiwango angedumu nacho naamini mwisho wa msimu huu Ajib angekua South
Africa mamelod sundown, Orlando pirates, kaizer chief, DRC Congo tp mazembe, au
misri Zamalek, au al ahly na huko angeitafuta vyema safari ya Old Trafford, San
siro, Allianz arena au wanda metropolitano.
Vyombo vya
habari vya Tanzania vimemtangaza vilivyo Ajib wa yanga, kuliko alivyokua simba.
Na kuna baadhi ya watangazaji waliwai kuchumpa
mipaka kwa kumpa sifa za kutisha kama vile kushushwa kutoka mbiguni, pia mtoto
wa Mungu.
Ajib
akajiona kama aliyeonja pepo, na aliamini ameshafanikiwa kuwakosoa simba sc.
Baada ya
mchezo wa yanga dhidi ya singida, Ajib ameshuka kile kiwango cha michezo sita
ya awali, athari yake imekua ndogo, huwenda anajiamini udhaifu wa kikosi cha
yanga unamtia kiburi aone hakuna wakumuweka benchi, Huwenda angekua bora kama
angekutana ya yanga ya moto wa gesi ikiwa na msuva, ngoma, kamusoko, niyonzima,
tambwe, bosou, dida, chini ya Hans pluijm lakini hawa wote hawapo katika
utimamu kama wa miaka mitatu iliyopita.
Na wengine wameshaachana na klabu hiyo.
Ajib
anaamini ameshaionesha simba sc na wameshajutia juu ya kumuacha, hivyo amerudi
katika kitanda chake kile kile alichokua analalia akiwa simba ili aendelee na
usingizi wake,nilichojifunza ni kwamba Ajib ana pande mbili za shilingi akiamua
anafanya makubwa asipoamua atawaudhi.
Siku njema.
Post a Comment
karibu kwa maoni