Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba PRC Shehan Mohd Shehan amseama , tukio hilo limetokea huko Semewani wilaya ya chakechake kusini Pemba ambapo mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo katika mazingira ya kumvizia.
Shehan amesema , wazee wa mtoto huyo walimtilia mashaka mtoto wao kutokana na hali yake ilivyokua na baada ya kumtazama waligundua kuwa ameingiliwa kimwili na walipomuuliza, mtoto alimtaja kijana huyo Omar Hamad kuwa ndie aliyemfanyia unyama huo.
” mtuhumiwa amekimbia na mpaka hivi sasa hajuulikani wapi alipo ” alisema Kamanda huyo.
Kamanda Shehan ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa huku akisema kuwa vitendo hivyo si vya kiutu na ifaaa kupigwa vita kwa hali ya juu.
Post a Comment
karibu kwa maoni