Mbunge
wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu' amelitetea Jeshi la Magereza
mbele ya Bunge kuwa jeshi hilo lina matatizo makubwa ya kiusafiri
jambo ambalo linapelekea wafungwa kupelekwa Mahakamani kwa miguu kitendo
ambacho kina hatarisha usalama wa mfungwa na askari kiujumla.
Kauli
hiyo ya Sugu imetolewa jana Mei 22, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye
kikao cha 34 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
"Pamoja
na matatizo waliyokuwa nayo Jeshi la Polisi katika masuala ya vyombo
vya usafiri lakini niwahakikishie Jeshi la Magereza lina hali mbaya
sana, hawana magari sio tu magari mabovu hawana magari kabisa, kiasi
kwamba wanafikia hatua ya kuwapeleka wafungwa ambao wanakesi Mahamani
kwa miguu huku wakiwa wamewafunga pingu. Hii ni mbaya sana kwa usalama
wa askari magereza pamoja na wale watuhumiwa ambao wamefungwa pingu",
alisema Sugu.
Pamoja
na hayo, Sugu aliendelea kwa kusema "mtu anatuhumiwa ujambazi halafu
anapitishwa mtaani kwa miguu wananchi wanamuona, wanaweza wakamvamia na
kumshambulia pamoja na kuhatarisha maisha ya mfungwa".
Kutokana
na ushauri huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba
akampongeza Mhe. Sugu kwa kusema "nimpongeze Mhe. Sugu kwa kuuliza swali
kwa experience, na niseme kwamba yeye ni mshauri mzuri. Tutalizingatia
hilo ili tuweke mgao kwenye upande wa Jeshi la Magereza ili kuepuka na
tahadhari aliyosema".
Post a Comment
karibu kwa maoni