Katika kuiunga
mkono serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli mkoa wa
Manyara umeendelea kuwa na viwanda vidogo vidogo vinavyotoa ajira kwa vijana.
Vilevile Mapunda amewataka vijana kuwa
wabunifu ili kuweza kukabiliana na changamoto ya ajira iliyopo hapa nchini
Akizungumza
na walter habari Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo [SIDO]
iliyopo Mtaa wa nyungu Wilayan Babati Mkoan Manyara
Abeli Mapunda amesema wanahudumia viwanda 2600
Mbali na viwanda
kazi nyingine zinazofanywa na SIDO ni kutoa mikopo katika vikundi mbalimbali
vinavyojihusisha na ujasiria mali
Hata hivyo Shirika
hili lipo chini ya wizara ya Viwanda,biashara na uwekezaji ikiwa imeanzishwa na
sheria ya bunge ya mwaka 1973.
Ikumbukwe kuwa
sera ya serikali ya awamu ya tano ni Tanzania ya Viwanda chini ya waziri mwenye
Dhamana ya viwanda Charles Mwijage ambaye amekuwa akiweka juhudi katika
kuhakikisha adhima hiyo ina fanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kujenga uchumi
imara wa Taifa kwa sababu hakuna nchi iliyo endelea kote ulimwenguni pasipokuwa
na viwanda vya kutosha.
Post a Comment
karibu kwa maoni